Hebrews 8:6-10

6 aLakini huduma aliyopewa Isa ni bora zaidi kuliko yao, kama vile agano ambalo yeye ni mpatanishi wake lilivyo bora zaidi kuliko lile la zamani, nalo limewekwa misingi wa ahadi zilizo bora zaidi.

7 bKwa maana kama hapakuwa na kasoro katika lile agano la kwanza, pasingekuwa na haja ya kutafuta nafasi kwa ajili ya jingine. 8 cLakini Mungu aliona kosa kwa watu, naye akasema: “Siku zinakuja, asema Bwana,
nitakapofanya agano jipya
na nyumba ya Israeli
na nyumba ya Yuda.

9 dAgano langu halitakuwa kama lile
nililofanya na baba zao
nilipowashika mkono
kuwaongoza watoke nchi ya Misri,
kwa sababu hawakuendelea kuwa waaminifu katika agano langu,
nami nikawaacha,
asema Bwana.

10 eHili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli
baada ya siku zile, asema Bwana.
Nitaziweka sheria zangu katika nia zao
na kuziandika mioyoni mwao.
Nitakuwa Mungu wao,
nao watakuwa watu wangu.
Copyright information for SwhKC